Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 3:31 pm

NEWS: SHIRIKA LA AMNESTY LALAANI GODBLESS LEMA KURUDISHWA TANZANIA

Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International limesema Kenya kutaka kumrudisha aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless lema nchini Tanzania ni kukiuka haki za kibinaadamu na kutotambua Sheria inayozuia kumrudisha mtu anayekimbia nchi yake kuepuka kushtakiwa.

Katika taarifa yao waliyoitoa kwa Umma, shirika la Amnesty international linalojihusisha na haki za kibinadamu limeona uwezekano wa mamlaka za Kenya kulazimika kumrejesha mwanasiasa wa upinzani, Godbless Lema au familia yake kwenye mateso ya kisiasa au uwezekano wa kufungwa Tanzania.

Mkurugenzi wa Amnesty International nchini Kenya, Irungu Houghton amesema kanuni ya kimataifa iliyoridhiwa na sheria za Kenya hairuhusu Kenya kuwarudisha watu kwenye mipaka kwenye nchi ambayo wamo kwenye mateso au hatari.

Karibuni, Godbless Lema alikimbila nchini Kenya na mkewe na watoto watatu akiomba hifadhi kutoka serikali ya Kenya. Lema na familia yake walivuka mpaka wa Namanga Novemba 8, 2020. Amnesty inaamini yupo chini ya polisi eneo la Kajiado, Kenya. Wakili wake, Prof. George Wajackoyah pia amethibitisha uwezekano wa kurejeshwa.