- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAWEKA PINGAMIZI KESI YA TOZO ZA SIMU
Dar es salaam. Serekali ya Tanzania imewasilisha pingamizi katika kesi na namba 11 ya mwaka 2021 ya kupinga tozo za miamala ya fedha katika Mitandao ya Simu na kutoa sababu zake tatu, huku ikidai kwamba shauri hilo halina msingi wowote maalum, hivyo anaomba lifutuliwe mablali.
Kesi ya kupinga tozo ya miamala ya simu iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) shauri la namba 11 la mwaka 2021 ilisikilizwa jana kwa mara ya pili saa nne (4) asubuhi.
Pingamizi hilo liliwasilishea jana Agosti 17, 2021 na wakili Mkuu wa Serekali Gabriel Mlata katika mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam mbele ya Jaji John Mgeta.
Akiwasilisha pingamizi alidai maombi hayana msingi kwa sababu hakuna uamuzi wowote uliyotolewa na walalamikiwa, ambao unahitaji kufutwa na mahakama,walichofanya walalamikiwa ni kutimiza wajibu wao kikatiba kutafuta chanzo cha mapato.
Mapingamizi hayo matatu yaliyoletwa na upande wa serikali unadai:
- Mahakama kuu haina uwezo wa kutoa nafuu zilizoombwa(untenable)
- Madai yamekosa sababu za msingi na
(iii) Madai hayo yamekosa ruhusa ya bodi ya mdai (Board Resolution).
Kesi hiyo imepangwa tena tarehe 08/09/2021 ambapo mahakama itatoa uamuzi kuhusu mapingamizi hayo.