- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAWATAKA WATANZANIA KUPUUZA KAULI YA PROF ASSAD
Dodoma. Serekali ya Tanzania imewataka Watanzania kupuuza maneno ya aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof.Mussa Assad kuhusu kauli yake Kuwa asilimia 60 ya watumishi wa Umma hawafai kuwepo katika nafasi zao na asilimia 40 wanao uwezo kidogo hivyo wale wasiofaaa wapigwe chini.
Kauli hiyo imetolewa jana April 14,2021 jijini Dodoma na KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Dkt.Laurean Ndumbaro wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa kauli iliyotolewa na Mstaafu huyo Wakati akihojiwa na waandishi wa habari inatia ukakasi kwa watumishi wa Umma na haina ukweli wowote .
JE KAULI YA ASSAD INAPASWA KUPUUZWA?
Prof Mussa Assad ni aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serekali ambaye ameongoza ofisi ile kwa ustadi mkubwa, amekagua mashirika na miradi mikubwa ya Serekali, amekagua karibu kila ofisi ya Serekali isipokuwa idara ya Rais yaani VOTE 20 ambaye haikaguliwi.
Inamaana Prof. Assad kwa kipindi chote hicho amekuwa akifanya kazi na watumishi wa Serekali karibu wote na wapo ambao amewahoji kwa mazungumzo na wapo ambao amewahoji kwa maandishi, kwahiyo kuna asilimia karibu 70 za ni kweli huenda anatambua ufanisi wa watumishi wa Serekali kupitia uzoefu alioufanya kama mkaguzi mkuu wa Serekali.