- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Serekali yatoa ufafanuzi wa Sababu Tatu za kupanda kwa bei ya sembe Nchini
Dar es salaam: Ufafanuzi huo ulitolewa jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi ili aweze kufafanua kuhusu kupanda kwa bei ya unga na hatua zinazochukuliwa na Serikali kudhibiti hali hiyo.
Japokuwa bei ya sembe imeendelea kupanda kwa miezi miwili sasa na kuzua hofu, Serikali imesema ni hali ya kawaida kwa miezi ya Desemba na Februari kila mwaka ila imepanga kuingiza sokoni unga kupitia Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi ili aweze kufafanua kuhusu kupanda kwa bei ya unga na hatua zinazochukuliwa na Serikali kudhibiti hali hiyo.
Ole Nasha alikuwa akitoa ufafanuzi wa habari ya uchunguzi iliyoripotiwa na gazeti la mwananchi hili jana kuhusu kupanda kwa bei ya sembe kutoka kati ya Sh800 na 1,000 kwa kilo adi kufikia Sh1,500, huku mfuko wa kilo 25 ukiuzwa Sh29,500 badala ya kati ya Sh22,000 na Sh24,000.
Uchunguzi wa Mwananchi uliofanywa kuanzia mapema mwezi uliopita umebaini kuwa mikoa maarufu kwa uzalishaji mahindi ya Ruvuma, Njombe, Mbeya na Rukwa imeingiliwa na walanguzi ambao wananunua mahindi na kuyasafirisha kwenda nchi jirani zenye uhaba wa chakula. Katika Mkoa wa Arusha bei ya unga na mahindi imepanda kutokana na kiasi kikubwa cha mazao hayo, kuuzwa nchi jirani ya Kenya. Katika masoko ya Kilombero na soko kuu la Arusha kwa sasa kilo moja ya unga inauzwa kati ya Sh1,100 na 1,300 kutoka kati ya Sh850 na Sh1,000 ya Juni mwaka huu
Vilevile, bei ya gunia moja imepanda kutoka Sh50,000 hadi kufikia Sh75,000 hali ambayo inatishia bei kupanda zaidi kabla ya kuanza kilimo na mavuno.
Kwa mujibu wa kitengo cha intelejensia ya biashara ya mazao cha nchini Kenya (RATIN) Juni mwaka huu Kenya ilinunua tani 13,103 za mahindi kutoka Tanzania.
Waziri Ole Nasha alikiri kuwa ni kweli bei ya unga wa sembe katika mikoa mbalimbali nchini imepanda lakini alisisitiza akisema kwa miezi hii ni jambo la kawaida na kwa mwaka huu inatokana na mazao ya vyakula yaliyovunwa msimu uliopita kukaribia kwisha hivyo wanasubiri kuvuna msimu mpya.
Pia, aliafikiana na uchunguzi wa Mwananchi akisema hali ya chakula kwa nchi jirani si nzuri hivyo baadhi ya wafanyabiashara hununua mazao ya vyakula na kusafirisha kwenda kuuza nje ya nchi. “Ndiyo maana katikati ya mwaka huu Serikali ilipiga marufuku uuzaji wa vyakula nje ya nchi ili kukabiliana na hali inayojitokeza sasa,” alisema.
Ole Nasha alitaja sababu nyingine kuwa ni tabia ya wafanyabiashara kuficha mazao hususani mahindi wakisubiri kuangalia hali ya hewa itakuwaje, kama kutakuwa na ukame wauze kwa bei ya juu na kama kutakuwa hakuna wauze kwa bei ya kawaida.
“Halijakuwa tatizo kubwa kiasi cha kuwachukulia hatua wanaofanya hivyo, iwapo hali itakuwa mbaya kuna sheria za kuwabana na ni rahisi kuwabaini pia,” alisema Ole Nasha.
source mwananchi