Home | Terms & Conditions | Help

April 4, 2025, 7:44 am

NEWS: SEREKALI YATOA RUZUKU YA BILIONI 100 KWENYE MAFUTA

Serikali ya Tanzania imetoa ruzuku ya TZS bilioni 100 kwenye mafuta ya petroli na Dizeli ili kupunguza makali ya bei ya bidhaa hiyo kuanzia mwezi June 1, 2022.

Akizungumza Bungeni wakati wa kutoa mkakati wa kukabiliana na kupanda kwa bei ya mafuta, hii leo Mai 10, 2022 Waziri wa Nishati January Makamba amesema

"Ruzuku hii (Shilingi Bilioni 100) inatolewa kwa kupunguza matumizi ya Serikali katika kipindi kilichobaki cha mwaka 2021/22.

Anaongeza kuwa Kutolewa kwa ruzuku hii hakutagusa miradi ya maendeleo ambayo inaendelea. Hatua hii imekuja baada ya Bunge la Tanzania wiki iliyopita kumpa Waziri huyo muda wa siku tano kuhakikisha anakuja na mkakati wa kupunguza bei ya mafuta ili kupunguza mzigo kwa wananchi.

Mbali na hatua hiyo Waziri huyo pia ameelezea mipango mingine ya kukabiliana na kupanda kwa bei ya mafuta ikiwemo kuruhusu watu wenye uwezo wa kuleta mafuta kufanya hivyo na kuwa na hifadhi ya mafuta ya kimakakati ambayo itawezesha kupata unafuu wa mafuta na mpango wa Ushirikiano wa kujenga maghala makubwa ya mafuta kwa ajili ya kuuza nje ya nchi.

Bei za mafuta zinaweza kupungua zaidi kuanzia Agasti 2022.