Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 2:24 am

NEWS: SEREKALI YATANGAZA KUSHUKA KWA MFUMUKO WA BEI

Serekali ya Tanzania imesema kuwa Mfumuko wa bei nchini kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2020 umepungua hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 3.1 kwa mwaka ulioishia Oktoba, 2020.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Desemba 8, jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth Minja.

Bi Minja amesema hali hiyo inamaanisha kwamba kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2020 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2020.

Amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2020 kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kupindi kilichoishia Novemba, 2019.

Aidha, amezitaja bidhaa hizo na asilimia kwenye mabano kuwa ni pamoja na mchele (4.5), mahindi (14.3), unga wa mahindi (5.7), unga wa mtama (4.4), viazi vitamu (2.6) vyakula vya watoto lishe (1.8) na ndizi za kupika (4.9).

Amesema kwa upande wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Novemba 2020 umepungua hadi asilimia 2.8 kutoka asilimia 3.4 kwa mwaka ulioishia Oktoba 2020.