Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 8:03 am

NEWS: SEREKALI YASITISHA KUKAGUA NYIMBO ZA WASANII

Dar es Salaam. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Imesitisha utaratibu wa Baraza la Sanaa Tanzania BASATA wa kukagua nyimbo za wasanii wote nchini kabla hazijapelekwa kwenye redio, televisheni na majukwaa mbalimbali ya kuchezwa nyimbo hizo.

Taarifa ya usitishwaji wa kanuni za kukagua nyimbo umetolewa leo hii Jumamosi Mei 8, 2021 na Waziri mwenye dhamana ya Sanaa Innocent Bashungwa alipokutana na wadau wa muziki nchini wakiwemo wasanii mkoani Dar es Salaam

Kanuni hizo ni za sheria namba 23 ya mwaka 1984 ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2019. Kanuni hizo namba 25 kifungu (1)-(8) inaeleza kuhusu masharti mahususi juu ya masuala ya maadili ya kazi za sanaa na utoaji wa ithibati katika kazi za sanaa.

Bashungwa amechukua uamuzi huo baada ya wadau wa muziki kupinga suala hilo wakidai haliwatendei haki ikiwa ni baada ya Basata kuzuia wimbo wa Mama wa msanii Ney wa Mitego kwa maelezo kuwa una mashairi yenye ukakasi..