- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAKIRI KIFO CHA ASKARI KWENYE MAPIGANO LOLIONDO
Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa Arusha, John Mongella ametoa taarifa juu ya kinachoendelea Loliondo na kusema kuwa askari mmoja wa Jeshi la Polisi amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kupigwa mshale na kundi la wananchi wenye silaha wakati wa zoezi la uwekaji wa alama za mipaka katika eneo hilo la Loliondo wilayani Ngorongoro.
Lakini RC Mongella ameuhabarisha umma wa Watanzania kuwa hali ya Loliondo kwasasa ni shwari sana na uwekaji wa mipaka katika eneo la kilometa 1,500 kwa ajili ya eneo nyeti la mazalia, chanzo cha maji na mapito ya wanyama kwenye eneo hilo.
Mongolla ameeleza hayo leo Jumamosi ya Juni 11, 2022 wakati akizungumzia kuhusu kinachoendelea katika eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro.
Mongella amesema kuwa kwa bahati mbaya jana alasiri askari mmoja aliuawa kwa kupigwa mshale na kundi la watu ambao lilitokea na kutaka kuathiri zoezi hilo na hata kuathiri utekelezaji wa zoezi hilo.
“Kwa bahati mbaya tu, alasiri ya jana (Ijumaa ya Juni 10, 2022) askari wetu mmoja aliuawa kwa kupigwa mshale na kundi la watu ambalo lilitokea na kutaka kuathiri na hata kuumiza wanaondelea na zoezi.
“Ni bahati mbaya sana, lakini askari huyu mzalendo tunatambua mchango wake na pamoja na kauli nzuri ya Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) bungeni jana asubuhi, lakini alasiri tulipata tukio hilo,” amesema Mongella.
Amesema kuwa kwa sasa zoezi hilo linaendelea vizuri na kwamba, baada ya kuweka alama kwenye maeneo hayo ni kuwa, mazoezi hayo yatakuwa shiriki kwa wananchi wote.
Amesema mpaka sasa kwenye maeneo na hospitali na vituo vya afya hakuna majeruhi, ingawa kwenye mitandao kuna picha zinatolewa na baadhi ni za miaka mingi iliyopita.
Amesema baadhi ya picha zimetambuliwa kuwa ni za miaka mitatu iliyopita na kwamba, kama kuna mtu ana jeraha kutokana na chochote ambacho anadhani kimesababishwa na mamlaka zetu basi ajitokeze ili apate huduma.
“Serikali yetu ni ya utawala wa sheria na msingi ya utawala bora na tungependa suala la upotoshaji lisiendelee. Tunafanya jambo la kimaendeleo kwa mustakabali wa wananchi wetu na jamii zetu na maslahi mapana ya nchi yetu,” amesema Mongela.