Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 8:25 pm

NEWS: SEREKALI YAKANUSHA KUSIMAMA BARABARA YA NJIA NANE

Serekali ya Tanzania imekanusha vikali taarifa iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikisema Mradi wa barabara ya njia 8 kutoka Kimara hadi Kibaha mkoani Pwani umekwama.

Taarifa hiyo imetolewa na msemaji mkuu wa wa Serekali Gernson Msigwa kupitia mitandao yake ya kijamii, na amefafanua kwamba mradi huo wa Kilometa 19.2 unakwenda vizuri na umefikia 94% na sasa unakamilishwa asilimia chache zilizobaki.

"Mradi wa ujenzi wa barabara ya njia nane ya Kimara - Kibaha yenye urefu wa kilometa 19.2 haujakwama kama ilivyochapishwa mtandaoni"

Amesema kuwa ujenzi wa mradi huo unakwenda vizuri na umefikia asilimia 94. Na kwamba malipo kwa makandarasi yanafanyika vizuri na ameshalipwa kwa zaidi ya asilimia 90 (takribani shilingi Bilioni 161).

"Kwa sasa kinachofanyika ni kukamilisha asilimia chache zilizobaki pamoja kuongeza mahitaji mengine ambayo hayakuwepo kwenye mkataba"

"Mapipa, uzi na kingo ambazo bado zipo barabarani ni kwa sababu za kiusalama kwa watumiaji wa barabara. Haina maana ujenzi umekwama" Alisema Msigwa.