Home | Terms & Conditions | Help

April 6, 2025, 7:12 pm

NEWS: SEREKALI YAJIPANGA KUJENGA VYUO 33

Rais Magufuli amesema kuwa Serikali hivi sasa inajenga vyuo vipya 33 vya VETA ambapo vinne vitakuwa ni vya ngazi ya mkoa na 29 ni vya ngazi ya wilaya, ambapo vitakapo kamilika ujenzi wake vitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 65 elfu na 640.

Rais Magufuli ameitoa kauli hiyo hii leo Januari 18, 2021 mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika chuo Cha VETA kinachojengwa kwa ufadhili wa serikali ya China, kwa gharama ya shilingi Bilioni 22 na amezindua rasmi shule ya sekondari ya Ihungo mkoani Kagera iliyojengwa upya baada ya kubomolewa na tetemeko.

Rais Magufuli ameeleza kuwa Miongoni mwa vyuo vipya vinavyojengwa ni pamoja na cha mkoa wa Kagera ambapo kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi kati ya 800 na 1000.

Aidha ameeleza kuwa ujenzi wa chuo cha VETA ni muendelezo wa mkakati wa serikali wa kujenga vyuo vya VETA kila mkoa nchini, kwani kwa sasa nchi ina vyuo vya VETA 712 ambapo vimeongezeka kutoka vyuo 672 mwaka 2015, kati ya vyuo hivyo vya serikali vipo 62 na 20 ni vya ngazi ya mkoa na 42 ni vya ngazi ya wilaya.