- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAAGIZA KUKAMATWA ASKOFU GWAJIMA
Butiama. Waziri wa Afya, nchini Tanzania Dk Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi nchini humo pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi wa nchi kuhusu chanjo ya Uviko 19.
Dk Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama akifafanua kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo ambalo linaloivuruga wizara yake ya Afya na Serikali ya Jamhuri katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Askofu Gwajima amekuwa akihubiri kanisani kwake shutuma dhidi ya viongozi wa Serekali na kuwaambia waumini wake kutochanjwa Chanjo ya Corona, hali ambayo inakwenda kinyume na Wizara ya Afya na Msimamo wa Rais Samia Suluhu Hassani
Gwajima amekuwa akisisitiza kuwa hatakubali kupatiwa chanjo ya kukabiliana na Uviko-19 na amekuwa akitoa kauli za kutoanekana kumuogopa mtu yeyote licha yakuwa anafanya upotoshaji.
Jumapili ya Juzi Askofu Gwajima alisema kuwa hana shida na ubunge baada ya kusambaa taarifa kutoka ofisi ya Bunge kwamba mbunge yeyote hataruhusiwa kwenda bungeni Bila chanjo.
Lakini baadae Ofisi ya Bunge ilikanusha taarifa hiyo lakini Spika wa Bunge, Job Ndugai akiwaasa wabunge kujitokeza kuchanja na kwamba japo ni hiyari lakini hakuna hiyari ya kuwaambukiza wengine Uviko-19.