- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAAGIZA HATI ZA ARDHI KUTOLEWA NDANI YA SIKU 7
TANGA. Serekali nchini Tanzania imeziagiza halimashauri zote nchini kutolewa Hati za umiliki wa ardhi ndani ya wiki pamoja pale mwananchi atakapokuwa amekamilisha taratibu zote za umilikishwaji ardhi.
Agizo hilo limetolewa jana Juni 22, 2020 na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeeo ya Makazi William Lukuvi wakati akizindua ofisi ya ardhi mkoa wa Tanga katika hafla fupi iliyofanyika jijini Tanga.
Uzinduzi wa Ofisi hizo ulihudhuriwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo.
Aidha Waziri Lukuvi ameagiza wananchi kupatiwa hati zao za ardhi katika halmashauri waliolipia gharama za kupatiwa hati ili kuondoa usumbufu pamoja na gharama kwa mwananchi kufuatilia Hati kwenye Ofisi za Ardhi za mikoa.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serekali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shighela, Kamishna wa Ardhi nchini Nathaniel Nghode, Katibu Tawala mkoa wa Tanga Judica Omari, Wakuu wa wilaya za mkoa wa Tanga pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali za mkoa wa Tanga.