- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI KUYAONDOA MADUKA YA DAWA NJEE YA HOSPITALI.
Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imewaagiza wamiliki wote wa maduka ya dawa nchini yaliyopo mita 500 kutoka kwenye vituo vya afya nchini kuyaondoa mara moja kabla ya Juni 30 mwaka huu.
Serekali imefafanua kuwa maduka hayo yapo kinyume cha kanuni ya famasia iliyowekwa mwaka 2020 hivyo wamiliki watachukuliwa hatua za kisheria kama wakikaidi.
Agizo hilo limetolewa hii leo Januari 24, 2022 na Waziri wa Afya, nchini Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake aliyoifanya katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo Upanga jijini Dar es salaam, kwa lengo la kuangalia ubora wa utoaji huduma kwa wagonjwa.
“Ninatuma salamu maduka yote ya dawa lazima yawe mita 500 kutoka ndani ya hospitali, tunakwenda kuyaondoa ifikapo Julai Mosi mwaka huu tulishatoa muda wa kutosha kufikia Juni 30 yawe yameondoka.
“Wamiliki wanafanya kinyume cha sheria nipo na mfamasia Mkuu wa serikali hapa, tulitunga na tulipitisha kanuni maduka yote yawe mita 500 kutoka hospitalini nikaambiwa waziri kuna wengine walipewa leseni kabla, hivyo tumebakisha miezi mitano hakuna cha msalie mtume wala kuomba radhi,” amesema Waziri Ummy.
"Mwananchi anakosaje dawa? Suala hili ni la pande mbili MSD na hospitali na nilishatoa maagizo. Uwepo wa haya maduka yanachangia udokozi wa dawa na yanaondoa imani kwa wananchi kwamba angalau kuna usimamizi mzuri wa dawa vituoni,” amesema Bi Ummy