- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI KUWASHUGHULIKIA WANAOVUNJA HAKI ZA WAFANYAKAZI
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Patrobas Katambi ametoa onyo kwa Waajiri wanaovunja haki za Wafanyakazi wa Ndani, wanaonyima mikataba wafanyakazi na wale wanaoajiri watoto wadogo kwa kusema kuwa Serikali inaendelea kuyafanyia kazi malalamiko yote yanayoifikia ofisi yake.
Katambi ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Vijana na kuahidi utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Rais Samia aliyoyatoa Zanzibar kuhusu Haki na Wajibu wa Vijana kwenye ujenzi wa Taifa huku akigusia haki za Wafanyakazi wa ndani.
"Wafanyakazi wa Ndani Domestic Workers ( VIJANA -Wakike na Wakiume) aghalabu Wanawake (Jeshi la Mama yetu Amiri Jeshi Samia Suluhu Hassan), pamoja na kuwa dunia ya leo ni ya Utandawazi lakini ndio wamegeuka Wazazi Walezi na Walimu Wakuu wa tabia na maaadili ya watoto wengi kizazi kipya Wanapitia mengi mazito: vipigo, kutengwa, kudhalilishwa na kubakwa, manyanyaso aina zote na ngono, dhuruma, mimba chini ya umri, n.k hata ulemavu na vifo"
"Sheria ya Ajira na mahusiano kazini (2004) RE 2019 inataka mtumishi awe na miaka 18 na 14 kwa masharti ilikutovunja kifungu Cha 5 (1)&(2) na 20(2) Sheria tajwa" Alisema Katambi.