- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI KUANZA KUWAKOPESHA WASANII PESA
Dar es Salaam. Serekali kupitia Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imeahidi kuanzia mwaka huu wa fedha,Wataanza utaratibu wa , kuwakopesha fedha wasanii wa Tanzania kwa ajili ya kurahisisha kufanya kazi zao, kilio ambacho kimekuwa cha muda mrefu.
Kauli hiyo imetolewa jana May 9, 2021 na Katibu mkuu wa Wizara hiyo Dk Hassan Abbas na kusema kuwa fedha hizo watazipata kupitia mfuko wa utamaduni wa wasanii, unaoanza kufanya kazi rasmi mwaka wa bajeti 2021/22.
“Tayari mfuko huo wa wasanii umepangiwa bajeti yake na kuanzia mwaka huu wa fedha wasanii mtaweza kunufaika nao ikiwamo kupata mikopo ya kuboresha kazi zenu.
“Hivyo ni wakati sasa wa wasanii kuwa karibu na vyama vyenu na taasisi zinazowasimamia wakiwamo Basata,Cosota na Bodi ya Filamu, ambao hawa watahusika kwa karibu katika kuratibu suala hili.”
Katibu huyo amesema kurejesha mfuko huo kutaondoa yale malalamiko ya mtu kuwa wazo na kushindwa kuliwazua kisa hana fedha.
Mfuko huo ulianzishwa Novemba 2019 katika kongamano la Sanaa la Mwalimu Nyerere lililofanyika mkoani Dar es Salaam, Waziri Mkuu siku hiyo aliuchangia Sh5 milioni huku hayati John Magufuli aliahidi kuuchangia Sh100 milioni katika uanzishwaji wake.
Katika hatua nyingine, katibu huyo aliitaka StarTimes kampuni itakayoonyesha tamthilia hiyo ya ‘We Men’ kuongeza vipindi vya Kiswahili na kueleza kuwa kwa sasa kazi za sanaa nyingi zimeboreshwa.
“StarTimes iendelee kuingia ubia na wadau mbalimbali, kuna vipaji vingi,kuna filamu nyingi, hivyo naamini vipindi vingi vya kitanzania vitaonyeshwa kwenye kisimbusi chenu. kwani naamini tumetoka kwenye ile ya jambazi kuvua viatu,”amesema Dk Abbas.
Meneja masoko StarTimes, David Malisa, amesema wamejipanga kukuza kazi za sanaa nchini na tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo jumla ya filamu 104 zimeonyeshwa huku Sh280 milioni zikiwa zimewekezwa kwa shughuli hiyo.
Max Rioba ambaye ni muandaaji wa tamthilia, amesema wamejitahidi kuiandaa filamu hiyo katika kiwango cha kimataifa na wanaamini italeta mapinduzi katika tasnia ya filamu kwa jumla.
Wasanii waliopo katika filamu hiyo ni pamoja na Max mwenyewe, Wema Sepetu, Shilole,Hemed Suleiman na Grace Mgonjo ambaye ni mke wa Profesa Jay