- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI KILIMANJARO YAKANUSHA KUWEPO KWA CORONA.
Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amekanusha vikali taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kufungwa kwa shule ya International School Moshi (ISM) kwa madai ya mwanafunzi mmoja kukutwa na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
Wakati huo huo pia Mkurugenzi wa shule hiyo, Anna Marsden ameomba radhi hii leo Januari 2021 kutokana na kusambaa kwa taarifa kuwa shule imefungwa na kusimamisha masomo, akisema ukweli ni kwamba masomo yanaendelea kama kawaida.
Mkanganyiko huo unaletwa na taarifa mbili tofauti zote kutoka katika shule hiyo, Chanzo cha taarifa za ndani kutoka katika shule hiyo zilizowekwa katika tovuti yake Januari 19,2021 ilitaarifu juu ya kuwepo kwa mwanafunzi aliyethibitika kuwa na Covid-19 na leo hii Mkurugenzi wa Shule hiyo amekanusha taarifa iliyochapishwa katika tovuti yao Rasmi.
Lakini Kwa mujibu sheria na maagizo ya Serikali ya Tanzania ni kwamba hakuna mtu mwingine kati ya viongozi wanne tu wanaotakiwa kutoa taarifa za Corona ambao ni rais, waziri mkuu, waziri mwenye dhamana ya afya na msemaji mkuu wa Serikali.
Bi Mghwira amesema kutokana na hali hiyo na baada ya taarifa kusambaa katika mitandao wa kijamii, alimtuma msaidizi wake pamoja na ofisa elimu wa mkoa ili waende katika shule hiyo kufahamu nini kilitokea.
Mkuu wa wilaya ya Moshi, Rajabu Kundya na meya wa manispaa ya Moshi, Juma Raibu kwa nyakati tofauti wamekanusha uwepo wa mwanafunzi aliyeathirika na virusi hivyo vya Corona.