- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI INAJENGA VITUO VYA AFYA 233
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amesema Serekali ya Rais Samia Suluhu Hassan inajenga vituo vya Afya 233 katika tarafa 107.
- Chongolo amesema ndani ya mwaka huu mmoja eneo muhimu la sekta ya afya limefikiwa kwa kiwango kikubwa kama ambavyo Ilani ya CCM imeahidi ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora na kuwawezesha kushiriki katika shughuli za maendeleo ya nchi.
Chongolo ametoa taarifa hiyo hii leo Machi 18, 2022 kuhusu mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassani.
"Hospitali za rufaa za mikoa 19 ziko katika hatua mbalimbali za kukamilisha ujenzi na ukarabati wake, kuna miradi ipatayo 127 ya ujenzi wa hospitali inaendelea katika halmashauri za wilaya nchini, halikadhalika kuna ujenzi wa vituo vya afya vipatavyo 233 katika tarafa 207, vyote hivi vina uwezo wa kufanya upasuaji, vikiwa na majengo ya OPD, Maabara na vichomea taka"
"Bila kusahau ujenzi wa zahanati zipatazo 564 katika halmashauri mbalimbali nchini ambao uko katika hatua za kukamilika, katika eneo la upatikanaji wa dawa ili kuondokana na malalamiko ya wananchi, mbali ya Serikali kutumia takriban Shilingi bilioni 333 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendenashi, inajenga viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba katika eneo la Idofi, Halmashauri ya Makambako, mkoani Njombe kwa lengo la kupunguza ununuzi wa dawa kutoka nje ya nchi.
"Hatua hii itasaidia kuimarisha upatikanaji wa dawa kwa wakati na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kwa ajili ya kununulia dawa nje ya nchi na hivyo fedha itakayookolewa itaelekezwa katika mipango mingine ya kuboresha huduma kwa wananchi"