- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI IMEYAFUTA MATOKEO YA MTIHANI WA UDKTARI ULIOVUJA
Dodoma. Serikali imeamua kuyafuta matokeo ya nadharia (theory) kwa masomo ya program ya Utabibu(udaktari) Ngazi ya Tano (NTA Level 5) baada ya kuabinika kuvuja kwa mitihani ya muhula wa pili wa programu hiyo kwa kwa kutumia mitandao ya kijamii kama Whatsapp na Telegram .
Akitangaza maamuzi hayo jijini Dodoma, leo Novemba 4, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifello Sichalwe amesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya uchunguzi wa kamati iliyoundwa kuchunguza viashiria vya uvujifu wa mitihani hiyo iliyofanyika ilifanyika 16 Agosti, 2021 hadi 30 Septemba, 2021.
“Wakati wa uchunguzi wa mitihani iliyovuja, kamati ilibaini kuwa mitihani hiyo ilisambazwa kupitia mitandao ya kijamii (telegram na WhatsApp) na kuonekena kwenye baadhi ya namba za simu za wanafunzi zilizofanyiwa uchunguzi na kamati.
Kupitia sheria ya Baraza Sura 129 na Kanuni za Mitihani, Kifungu 33 (1) (iii), 2004 limefuta matokeo ya mitihani ya nadharia (theory) kwa masomo yote ya Programu ya Utabibu Ngazi ya Tano na baraza limeagiza kurudiwa kwa mitihani hiyo upya ndani ya wiki Sita kuanzia tarehe Novemba 1, 2021,” amesema Dk Sichalwe.
Mganga Mkuu huyo pia amesema mitihani hiyo itafanyika sambamba na mitihani ya marudio (supplementary Exams) kwa program zingine za afya nchi nzima.