- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Sakata la faru John lachukua sura mpya baada ya kugundulika kuwa zaidi ya Maofisa 56 walishiriki kumuhamisha.
Arusha: SAKATA la kutoweka kwa faru John lililoibuliwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika mikoa ya Arusha na Manyara linazidi kuchukua sura mpya kila kukicha.
Habari kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kwamba mchakato wa kuhamishwa kwa faru John kutoka Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro kwenda Grumeti, ulianza katika eneo la Nyasirori ndani ya Hifadhi ya Serengeti Aprili 17, 2015.
Uamuzi huo kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika serikalini, ulianza siku hiyo hiyo wakati wa tukio la kuwafungulia mbwa mwitu waliokuwa wamehifadhiwa katika eneo maalumu huko Nyasirori.
Vyanzo vya uhakika vya habari vinaeleza kwamba mjadala kuhusu kuhamishwa kwa faru John ulifanyika wakati watendaji wakuu wa taasisi za uhifadhi za Serikali zinazounda Kamati Maalumu ya Kuwalinda Tembo na Faru (National Elephant and Rhino Steering Committee) wakiwapo.Miongoni mwa watendaji wanaotajwa kuwapo wakati wa mjadala kuhusu kuhamishwa kwa faru huyo kutoka katika Bonde la Ngorongoro kutokana na sababu za kitaalamu, ni Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), Dk. Fadhili Manongi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi.
Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI), Dk. Simon Mduma na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori aliyefahamika kwa jina la Alex Choya.
Taarifa kuhusu kuwapo kwa haja ya kuhamishwa kwa faru huyo zilipelekwa hadi Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kufikishwa kwa suala hilo wizarani kulifuatiwa na hatua ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Adelhem Meru, kuwaandikia barua watendaji wa Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro kutekeleza uamuzi huo ifikapo Desemba 31, 2015.
Alipoulizwa kuhusu uwapo wa barua hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema ni kweli barua hiyo ipo kwenye kumbukumbu za wizara.
“Ni kweli hiyo document ipo, lakini hili suala la faru John linafanyiwa kazi na vyombo vya dola. Nadhani si vizuri kulijadili kwa undani sasa, tusubiri matokeo ya uchunguzi,” alisema Waziri Maghembe.
Wahifadhi kadhaa waliozungumza na gazeti hili kutoka Serengeti na Ngorongoro juu ya sakata hilo, walieleza kwamba kiini cha kufikiwa kwa uamuzi huo kulitokana na mabadiliko makubwa ya kitabia aliyokuwa nayo faru John tangu mwaka 2002.
“Faru John alizaliwa ndani ya Ngorongoro, na alianza kuonyesha tabia za ukorofi dhidi ya faru wengine madume mwaka 2002,” alieleza mhifadhi mmoja anayefanya kazi Ngorongoro.
Mhifadhi mwingine alimweleza mwandishi wetu kwamba hali hiyo ilisababisha Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro kufanya mawasiliano na TAWIRI kuhusu hatua za kuchukua.
Alisema kuwa hali ilizidi kuwa mbaya na mwaka 2005 kiliitishwa kikao kingine kujadili matatizo ya faru John ambaye tabia yake ya kuwapiga faru wengine ilisababisha wanyama hao kutoka ndani ya Ngorongoro na hivyo kusababisha ugumu wa kuwalinda.
“Tatizo jingine lililotokana na ubabe wa faru John, ni gharama kubwa za ulinzi wa faru waliokimbia vipigo, na kutawanyika hadi kwenye mashamba ya watu.
“Faru wana tabia moja, pindi wanapopigana, yule aliyeshindwa huondoka eneo husika,” alieleza mhifadhi mwingine aliyezungumza na MTANZANIA.
Taarifa kutoka Ngorongoro zinaeleza kuwa mwaka 2013 tatizo la faru John lilizidi kuwa baya zaidi pale kreta, baada ya faru huyo kuua wenzake wawili.
Katika tukio hilo, faru John anatajwa aliua ndama (jike) kwa kumchoma na pembe na kisha akaua dume mwenzake katika mapigano.
Mhifadhi huyo aliliambia gazeti hili kwamba faru John ndiye aliyekuwa na watoto wengi katika Bonde la Ngorongoro kuliko faru mwingine yeyote.
Tukio la faru John kumuua ndama kwa pembe lilitokea wakati alipokuwa akijaribu kumpanda mama yake.
“Faru John alianza kuwapanda watoto wake, jambo ambalo kitaalamu si salama kwa uhai wa faru, hivyo kuendelea kumwacha pale kreta lilikuwa jambo la hatari.
“Baada ya matukio hayo ya 2013, kikao kilikaa tena ambapo TANAPA pia walihudhuria, swali kubwa likiwa ni wapi ambako faru John alipaswa kupelekwa?” alisema mhifadhi mwingine.