- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SABAYA NA WENZAKE WAACHILIWA HURU NA MAHAKAMA
Arusha. Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha hatimaye imewaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita baada ya mahakama hiyo kuona kuwa ushahidi uliotolewa na Jamhuri kugubikwa na utata, hivyo kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yanawakabili na kuwatia hatiani.
Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha, Nathan Msuya na Sabaya mwenyewe.
Hata hivyo Sabaya, Nyegu, Aweyo na Msuya wataendelea kubaki mahabusu katika gereza la Karanga kwa kuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.
Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Juni 10 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo.
Kwasasa Sabaya atakuwa ameshinda kesi mbili ambapo Mei 6, 2022 akiwa na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, walishinda rufaa iliyokuwa ikisikilizwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, waliyokata kupinga hukumu ya miaka 30 iliyokuwa imetolewa na na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
Hakimu Kisinda amesema kuwa mbali na sababu hizo, mahakama imegundua kuwa hati ya mashitaka ilikuwa na mapungufu na kuwa ushahidi uliotolewa dhidi yao mahakamani hapo haujaweza kuthibitisha mashtaka hayo.