- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SABAYA NA WENZAKE WAACHILIWA HURU
Mahakama Kuu imemuachia huru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baada ya kubaini kulikuwa na mapungufu katika mwenendo mzima wa kesi, pamoja na kutofautiana kwa mashahidi.
Kesi hiyo iliyokuwa ikiwakabili Sabaya na wenzake wawili, ambao ni Sylivester Nyengu (26) na Daniel Mbura(38), ambao walifungwa miaka 30 jela na Hakimu Mwandamizi, Odira Amworo, baada ya kukutwa na makosa ya kutishia kwa silaha, kuteka na kunyang’anya fedha zaidi ya Sh milioni 2.7.
Sabaya na wenzake walikata rufaa kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
Rufaa hiyo ilisikilizwa kuanzia Februari 14 mwaka huu hadi Februari 21, ambapo hoja 14 za waleta rufaa wakidai Hakimu Mfawidhi Mwandamizi, Amworo, alikosea kisheria kutoa adhabu hiyo ya miaka 30, kwani ushahidi uliotolewa dhidi yao hauna msingi.
Jaji aliyekua akisikiliza rufaa hiyo, Ezedekia Kisanya amesema kulikuwa na mkanganyiko kwenye usikilizwaji wa kesi hiyo ikiwemo kutofautiana kwa mashahidi na kuufanya ushahidi kuwa batili. Pia Jaji Kisanya amesema mshtakiwa namba mbili Silvester Nyegu na namba tatu Daniel Mbura hawakupewa haki ya kumhoji Shahidi namba mbili wa Jamhuri hali iliyowayimwa haki yao msingi kishwria. Hivyo Jaji Kisanya amebatilisha hukumu iliyotolewa na mahakama ya Hakimu mkazi Arusha na kuwaachia washtakiwa wote watatu huru.
Hata hivyo pamoja na kuachiwa huru, Sabaya na washtakiwa wenzake wamerudishwa gerezani Kisongo, kwa sababu wanakabiliwa na kesi nyingine ya "ujambazi" wa kutumia silaha, wakituhumiwa kumshambulia mfanyabiashara Francis Mrosso. Kesi hiyo inatarajiwa kutolewa hukumu May 30 mwaka huu.
Jaji Kisanya amesema amewaachia huru washtakiwa wote watatu, lakini hawataweza kwenda nyumbani kwa sababu wana kesi nyingine kwenye Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha, na hivyo watarudi gerezani Kisongo hadi kesi hiyo itakapotolewa hukumu.
"Mngeweza kuwa huru kama msingekuwa na kesi nyingine katika mahakama yoyote nchini, lakini kwa kuwa mna kesi katika nyingine, mtarudi gerezani (Kisongo) mpaka kesi hiyo itakapotolewa hukumu" amesema Jaji Kisanya.!