- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SABAYA KURUDI MAHAKAMANI KWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI
Arusha. Pepo la kesi linaendelea kumuandamana aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita mara baada ya kesho Jumatatu, kutarajiwa kurejea tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza kesi yao nyingine ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya kuendesha genge la uhalifu na utakatishaji wa fedha inayowakabili.
Sabaya anatumikia kifungo cha miaka 30 Jela mara baada ya kutwa na kesi ya unyang'anyi kwa kutumia silaha.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi Octoba 15, 2021 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo.
Hakimu Amworo alisema kuwa mahakama imejiridhisha kuwa siku ya tukio February 9 mwaka 2021 washtakiwa wote watatu walikua dukani kwa Saad na wote walishiriki kufanya unyang'anyi wa kutumia silaha, kabla ya kumpiga Saad na kumsabanishia majeraha, wakitaka wapewe TZS 100M au mfanyabiashara huyo apewe kesi ya uhujumu uchumi.
Hakimu anasema kwa mujibu wa kifungu cha 201 cha sheria ya makosa ya adhabu, mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kutumia silaha kunyang'anya mali ya mtu mwingine, adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela pamoja na viboko 12 au miaka 30 bila viboko