Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 7:59 pm

NEWS: SABAYA AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Arusha. Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Arusha imewakuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, na wenzake wawili Sylevester Nyegu, Daniel Mbura, kwamsingi huo watatu hao wanatakiwa kuanza kujitetea kesho Ijumaa Agosti 13, 2021.

Sabaya na wenzake wawili wanatuhumiwa kutenda makosa matatu ya unyang’anyi wa kutumia silaha ambapo makosa hayo waliyatenda katika duka la Bw. Mohamed Saad huko eneo la Bondeni jijini Arusha, Februari 9 mwaka huu.