- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SABABU ZA BARCA KUSHINDWA KUMRUDISHA MESSI
HISPANIA. Jana club ya Barcelona ilitangaza kinyonge taarifa ya kuondoka kwa Mshambuliaji wake Leonel Messi hii ni baada ya club hiyo kushindwa kuendelea na Messi kutokana na kubanwa na Sheria za Kifedha na za kimfumo zilizowekwa katika ligi ya la Liga miaka 8 iliyopita.
Jana asubuhi Messi na Baba yake Jorge waliwasili Camp Nou ili kusaini kandarasi mpya mpaka June 2026 lakini kutokana na kanuni hizo za LA LIGA (SPAIN LA LIGA REGULATIONS) dili hilo likafeli.
Makubaliano baina ya Messi na Barcelona yalikuwa yameshafikiwa tangu Juni 30, 2021 lakini ilikuwa imebaki namna watakavyo weza kurekebisha muundo wa club.
Ligi kuu na Ligi daraja la kwanza walisaini sheria tangu 2013 za kuhakikisha klabu zote zinakuwa na kiwango cha matumizi kwa mishahara ya Wachezaji na Makocha
Kutokana na suala hilo, Barcelona wamevuka kiwango kinachotakiwa na inasemekana sio Messi pekee bali Wachezaji wengi wa klabu hiyo wanashindwa kuwaingiza kwenye mfumo mpaka baadhi ya wachezaji wapungue kwa kuuzwa.
Kutokana na tatizo hilo, club ya PSG tayari wameanza mazungumzo ya haraka ya kumnasa Lionel Messi ikiwa ni baada ya Messi kugoma mara ya kwanza kujiunga na Miamba hiyo ya Ufaransa.