- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RPC SHANA APONEA CHUPUCHUPU KUTUMBULIWA NA MAGUFULI
Rais waTanzania, John Pombe Magufuli amemuonya vikali Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shana kutokana na kufanya Kazi zake binafsi badala ya zile alizoagizwa kufanya na yeye kama mteule wake.
Onyo hilo amelitoa hii leo Juni 22, Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua ambapo amesema kuwa ameamua kumsamehe Kamanda Shana pamoja na Afisa wa TAKUKURU mkoani humo lakini wamesamehewa kwa sharti moja tu, la kutofanya kosa lolote tena.
"IGP na Mkurugenzi wa TAKUKURU mko hapa, mkawaambie watendaji wenu walioko Arusha wafanye kazi nilizowatuma, nao leo nilikuwa niwatoe RPC na Mkuu wa TAKUKURU wa Arusha", amesema Rais Magufuli.
"Nimeamua kuwasamehe lakini sijawasamehe moja kwa moja wakifanya kosa lolote wataondoka. Wakafanye kazi nilizowatuma wasifanye kazi wanazojituma wao, haiwezekani watu umewatuma kufanya kazi za serikali wanafanya kazi wanazozijua wao", ameongeza.
Katika tukio hilo, Rais Magufuli amemuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha mteule, Idd Kimanta pamoja na kushuhudia uapisho wa wakuu wawili wa wilaya ya Monduli, ACP Jotham Balele na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa.