- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RC MTAKA AOMBA RADHI KWA MANENO YAKE
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ameomba Radhi kwa viongozi wenzake na wananchi kwa ujumla wake kutokana na kauli yake aliyoitoa siku za hivi karibu ya kwamba wananchi wasisikilize kauli ya Waziri juu ya kuwepo kwa kambi za kitaaluma katika mkoa wa Dodoma kwa wanafunzi wa Kidato cha nne na sita ambao wanajiandaa kwa mitihani ya Taifa.
Haya ndio maneno aliyosema “Watoto wasome, msisikilize ushauri wa Watu wanaowaambia kwamba kambi zisiwepo, watoto hao hawasomi shule za kata, wanasoma shule za ada milioni 10, maana yangu ni kwamba usisikilize ushauri wa Waziri anaekwambia kusiwe na kambi”
Mtaki aliongea maneno ya hayo na wanchini wa Dodoma akiwahimiza kuzingatia Masomo ya watoto wao ili wapate kufaulu na kujikomboa na adha ya maisha.
Baada ya video yake hiyo akiongea na Wananchi kusambaa na kupokea maoni mbalimbali, RC Mtaka ameandika yafuatayo.
“Nimesoma na kupokea maoni, ushauri na kila aina ya hisia ambazo naamini ni kwa upendo juu ya Clip yangu kuhusu kambi za Kitaaluma nilipokuwa nikizungumza na Wananchi wetu katika tafsiri yoyote ile naomba radhi kwa wote waliokwazika, Wananchi na Viongozi wenzangu hasa pale matumizi ya neno "Waziri" lilipobeba hisia tofauti”
“Nawaheshimu Mawaziri wote na nafanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa natambua pia kazi nzuri inayofanywa na Mawaziri wetu wanaosimamia sekta ya elimu, wapo wanaodhani maelezo ya hisia zangu ni kuanza kupandisha mabega na pengine mgema akisifiwa tembo hutia maji, niwaondoe hofu sina sababu ya kupandisha mabega”