- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RC MTAKA ALAANI VIKALI TUKIO LA MAUWAJI YA WATU 5 DODOMA
Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amelitaka Jeshi la Polisi mkoani humo kuanza Uchunguzi mara moja kubaini watu wote waliohusika na kufanya mauaji ya watu watano wa familia moja waliouwawa kikatili wilayani Bahi.
RC Mtaka ametoa agizo hilo hii leo Janurai 23, 2022 alipofika eneo la tukio Kijiji cha Zanka,Wilayani Bahi, Mkoani Dodoma na kushuhudia miili ya marehemu hao watano wa familia moja ambao wameuawa kikatili
Mtaka amesema kuuawa kwa watu hao watano sio tukio la kuchunguzwa na watu wa Wilaya ya Bahi ni vyema vikosi vyote vishirikiane ili kubaini ni nani ambaye amefanya tukio hilo la kinyama
"lazima hawa watu wapatikane, ni lazima labda wanazanka wawe wanafiki mko tayari muwe wanafiki, mwenyekiti wa kijiji naomba wananchi wako washirikiane kwenye hili jambo" amesema Antony Mtaka