- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RC DAR AWAPATANISHA MEYA NA MKURUGENZI WALIOGOMBANA
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amefanikiwa kutatua uhasama baina ya meya manispaa ya kinondoni Songoro Mnyonge na mkurugenzi wa manispaa hiyo Bi Spora Liana mara baada ya viongozi hao kupishana kauli kiasi cha kutaka kuvunjiana heshima katika kiao cha Madiwani cha Manspaa hiyo.
Utatuzi wa mgogoro huo umefanyika leo katika kikao Cha pamoja kilichoitishwa leo na mkuu wa mkoa na kuwakutanisha meya na mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni.
Mkuu wa mkoa amewataka viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.
"Kwa upande wa Meya na mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya wananchi" -amesema Amos makalla