- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS ZUMA AGOMA KUJISALIMISHA KWA POLISI
Afrika Kusini. Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ambaye aliyeagizwa na vyombo vya Usalama kujisalimisha mwenyewe kwa polisi ili kuanza kifungo cha miezi 15 jela kwa kupuuza na kutoheshimu amri ya mahakama, amesema hatajisalimisha kamwe mpaka kufikia muda wa mwisho uliowekwa na Mahakama.
Zuma amewaambia waandishi wa habari katika makaazi yake ya Nkandla, wilaya ya Kwa-Zulu Natal kuwa hakuna haja ya yeye kwenda jela.
Amesema atakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya kumpa adhabu ya kifungo cha miezi 15 jela pamoja na kuzuia agizo la kukamatwa kwake na polisi.
Rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 79, amesema kupelekwa jela wakati wa kilele cha janga la ugonjwa wa Covid-19 ni sawa na kuhukumiwa kifo.
Zuma amewaambia maelfu ya wafuasi wake waliokuwa wamekusanyika nje ya makaazi yake ya Nkandla kuwa alinyimwa haki zake za kikatiba na majaji wa mahakama ya katiba nchini humo.
"Siombi kuonewa huruma lakini nataka haki. Umri wangu na hali yangu ya kiafya pamoja na mambo mengine hayakuzingatiwa wakati uamuzi ulipotolewa."