Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 7:35 pm

NEWS: RAIS WA VENEZUELA MADURO AMTIMUA BALOZI WA UMOJA WA ULAYA

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametoa muda wa saa 72 kuanzia Jana kwa balozi wa Umoja wa Ulaya nchini humo awe ameondoka katika ardhi ya Venezula kabla hatua kali hazijachukuliwa.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, ameuomba Umoja wa Ulaya kutoingilia masuala ya ndani ya nchi yake.

Uwamuzi huo wa Rais Maduro unakuja mara baada ya Umoja wa Ulaya, EU, kuliwekea vikwazo kundi la wawakilishi wa Venezuela kwa hatua zao dhidi ya baraza la Congress ambapo upinzani una viti vingi.

Wakati huo huo Umoja aw Ulaya umelaani hatu hiyo ya kufukuzwa kwa balozi wake nchini Venezuela.

Mkuu wa sera ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amelaani hatua hiyo ya rais wa Venezuela na kutangaza hatua za "kukabiliana" na uamuzi huo.

"Tunalaani na tunafutilia mbali hatua hiyo ya kufukuzwa kwa balozi wetu huko Caracas na tutachukua hatua za kukabiliana na uamuzi huo," Josep Borrell amesema katika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter.