- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA UKRAINE AOMBA MAZUNGUMZO NA URUSI
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy leo Machi 19, 2022 ameomba kufanyika kwa mazungumzo ya kina ya amani na Serekali ya Moscow, akisema ndiyo nafasi pekee ya Urusi kupunguza uharibifu uliotokana na makosa yake baada ya kufanya uvamizi nchini humo.
Zelenskiy amesema Ukraine imekuwa ikitoa suluhisho kila wakati la amani na kutaka mazungumzo yenye maana juu ya usalama bila kuchelewa.
Kulingana na Zelenskiy vikosi vya Urusi vinazuia kwa makusudi usambazaji wa misaada ya kiutu katika miji iliyoko chini ya mashambulizi.
Wakati huo huo vikosi vya Urusi vimezidisha mashambulizi katika miji ya Ukraine ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Kyiv na kituo cha ukarabati wa ndege nje kidogo ya mji wa Lviv, karibu na mpaka na Poland