Home | Terms & Conditions | Help

April 4, 2025, 7:46 am

NEWS: RAIS WA UKRAINE AMFUTA KAZI MKUU WA USALAMA WA TAIFA NA MWENDESHA MASHTAKA

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemuondoa kazini mkuu wa shirika la usalama la Ukraine (SBU) na mwendesha mashtaka mkuu wa nchi hiyo, akitaja visa vingi vya uhaini katika mashirika hayo mawili yenye nguvu.

Alisema zaidi ya wafanyakazi 60 wa zamani sasa wanafanya kazi dhidi ya Ukraine katika maeneo yanayokaliwa na Urusi.Jumla ya kesi 651 za ushirikiano na uhaini zilikuwa zimefunguliwa dhidi ya maafisa wa kutekeleza sheria, aliongeza.

Maafisa waliofutwa kazi, Ivan Bakanov na Iryna Venediktova, hawajatoa maoni yoyote.Katika hotuba yake ya video usiku wa Jumapili, Bw Zelensky alisema: "Msururu kama huo wa uhalifu dhidi ya misingi ya usalama wa taifa... unazua maswali mazito sana kwa wakuu husika [wa mashirika hayo mawili].

"Kila moja ya maswali haya yatapata jibu sahihi," rais wa Ukraine aliongeza.

Kufutwa kazi kwa mkuu wa SBU Ivan Bakanov, rafiki wa tangu utotoni wa Bw Zelensky, kunafuatia kukamatwa kwa mkuu wa zamani wa SBU katika eneo la Crimea, ambako kulitwaliwa na Urusi mwaka wa 2014. Oleh Kulinych anashukiwa kwa uhaini.