- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA SYRI LANKA ANAJINDAA KUKIMBILIA UHAMISHONI
Taarifa kutoka nchini Sri Lanka zinasema kuwa rais wa taifa hilo anayekabiliwa na mzozo amesafirishwa hadi kituo cha jeshi la wanaanga na kuibua uvumi kwamba huenda akakimbilia uhamishoni.
Rais Gotabaya Rajapaksa alikimbia Ikulu mjini Colombo chini ya ulinzi mkali wa wanajeshi wa majini siku ya Jumamosi, muda mchache baada ya maelfu ya waandamanaji kuvamia majengo ya Ikulu. Afisa mmoja mwandamizi wa kijeshi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Rais huyo mwenye umri wa miaka 73 amechukua hifadhi katika kituo kimoja cha kijeshi kabla ya kupelekwa kwenye kambi ya anga ya Katunayake inayopakana na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bandaranaike.
Hapajakuwa na tarifa rasmi kutoka ofisi ya rais juu ya wapi alipo kiongozi huyo, lakini ripoti za vyombo vya habari vya Sri Lanka zinaashiria kwamba Rajapaksa huenda akakimbilia Dubai baadae leo.
Spika wa bunge Mahinda Yapa Abeywardena amesema bunge litakutana tena Julai 15 na rais mpya atachaguliwa Julai 20 wakati rais Rajapaksa akijiandaa kuachia mikoba siku ya Jumatano. Spika Mahinda ameongeza kuwa "katika kikao cha viongozi wa chama kilichofanyika leo, ilikubaliwa kwamba hatua hii ni muhimu ili kuhakikisha serikali mpya ya vyama vyote inapatikana kwa mujibu wa Katiba na kuendeleza huduma muhimu."
Kwa upande wake, kiongozi wa upinzani Bw Sajith Premadasa ambaye chama chake cha Samagi Jana Balawegaya SJB kinashikilia viti 54 katika bunge lenye jumla ya viti 225 amesema kuwa wako tayari kuunda serikali. Amesema kama upinzani wako tayari kutoa uongozi ili kutuliza nchi na kujenga uchumi. "Tutachagua rais mpya, waziri mkuu mpya na kuunda serikali". Chama hicho cha SBJ kimekuwa katika mazungumzo na makundi ya vyama vidogo ili kupata uungwaji mkono wa kiongozi wao Premadasa.