- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA SOMALIA AMFUTA KAZI WAZIRI MKUU WAKE
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed maarufu kama 'Farmajo' amemsimamisha kazi Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble, ambaye ndiye aliongoza mchakato wa uchaguzi, kufuatia madai ya "ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka."
Kusimamishwa kwa Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble kunakuja siku moja baada ya Waziri Mkuu huyo kumshutumu Rais Farmajo kwa kufanya njama katika uchaguzi wa bunge wa nchi hiyo.
Rais Farmajo anataja Kifungu cha 87 cha Katiba ya Muda ya Somalia na sheria iliyowekwa Januari 18, 20 ya miaka 20 kuhusu ulinzi wa ardhi ya umma wakati wa uchaguzi wa Oktoba 27, 2021.
Msemaji wa Rais Mohamed, maarufu Farmajo, alisema rais alichukua hatua hiyo kutokana na uchunguzi wa ununuzi haramu wa ardhi ya umma unaomhusisha Waziri Mkuu Roble. Wakati duru nchini Somalia zinadai kuwa Kusimamishwa kwa Roble kunakuja siku moja baada ya Waziri Mkuu huyo kumshutumu Rais Farmajo kwa njama katika uchaguzi wa bunge.
Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba vikosi vya usalama vimepelekwa kuzunguka ofisi za Roble, ambapo waziri mdogo wa habari nchini humo anaelezea kama mapinduzi yasiyo ya moja kwa moja. Viongozi hao wanaozozana walikuwa wamefikia makubaliano mapema mwaka huu ambayo yangeruhusu wajumbe 101 kuchagua wabunge ambao wangemchagua rais ajeye.