- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA MEXICO AAMBUKIZWA CORONA
Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez ametangaza kuwa ameambukizwa virusi vya Corona usiku wa kuamikia leo.
Lopez anayefahamika zaidi kwa kupuuzia janga la virus vya Corona ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba amegundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona lakini anaonesha dalili za kawaida na tayari ameanza kupatiwa matibabu.
Amesema ana matumaini ya kupata nafuu na ataendelea na shughuli za kila siku za kuongoza taifa ikiwa ni pamoja na mazungumzo ya simu na rais Vladimir Putin wa Urusi yaliyopangwa kufanyika baadae hivi leo.
Kwa muda mrefu kiongozi huyo ameonesha kutolipa uzito janga la virusi vya corona na mara nyingi huonekana hadharani bila ya kuvaa barakoa.
Mexico imepoteza zaidi ya watu 149,000 kutoka na ugonjwa wa COVID-19 na kuwa taifa la nne duniani kwa idadi kubwa ya vifo tangu kuzuka kwa janga hilo mwishoni mwa mwaka 2019.