- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA MALI AJIUZULU NA KULIVUNJA BUNGE
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, amelazimika kujiuzulu na kulivunja bunge saa chache tu baada ya waasi wa jeshi la mali kumkamata na kumzuilia pamoja na maafisa wa ngazi ya juu katika serikali yake akiwemo Waziri mkuu wa nchi hiyo.
Katika hotuba fupi kupitia televisheni ya taifa Keita alisema “sitaki damu imwagike ili niendeleaa kuwa mamlakani”.
Asubuhi ya jana Jumanne wanajeshi walioasi katika mji mkuu wa Mali walimkamata Keita na Waziri Mkuu, Boubou Cisse na waliwaweka kizuizini.
Ripota wa Idhaa ya Kifaransa ya Sauti ya Amerika anasema rais alikamatwa akiwa nyumbani kwake huko Bamako na alichukuliwa hadi kambi ya jeshi katika mji unaoitwa Kati uliopo kiasi cha kilomita 15. Waziri Mkuu Cisse naye alipelekwa kwenye kambi hiyo hiyo.
Milio ya risasi ilizuka kwenye mji uitwao Kati mwanzoni mwa siku. Ripota aliyeko Mali aliiambia VOA kwamba wanajeshi waliingia katika mapigano, walichukua bunduki na kuanza kufyatua risasi hewani, waliingia mtaani na kufunga njia kuelekea kwenye kambi hiyo.
Hakuna vifo vyovyote vilivyoripotiwa katika ghasia hizo. Uasi katika kambi hiyo hiyo ulichochea mapinduzi dhidi ya Rais wa Mali, Amadou Toumani Toure mwaka 2012