- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA KOREA KUSINI AMPA MSAMAHA RAIS WA ZAMANI WA NCHI HIYO
Rasi wa sasa nchini Korea Kusini Moon Jae-in imetangaza kumpa msamaha maalum Rais wa zamani wa nchi hiyo Park Geun-hye, ambaye alihukumiwa kifungo cha muda mrefu jela kutokana na mfululizo wa mashtaka ya rushwa na uhujumu uchumi yaliyomkabili.
Kwamujibu wa Wizara ya Sheria ya Korea Kusini imesema msamaha wa Park unalenga kukuza umoja wa kitaifa katika kukabiliana na matatizo yaliyosababishwa na janga la virusi vya corona. Rais huyo wa zamani anatarajiwa kuachiwa kabla ya mwaka huu kumalizika.
Park alikamatwa na kupelekwa gerezani mnamo mwaka 2017, baada ya kuondolewa madarakani kutokana na kashfa ya ufisadi hali iliyosababisha maandamano makubwa kwa miezi kadhaa. Miongoni mwa mashtaka makuu yaliyomkabili yalikuwa ni kula njama na rafiki yake wa muda mrefu, Choi Soon-sil, ambapo walishirikiana kuchukua rushwa ya mamilioni ya dola pamoja na kupokea fedha kutoka kwenye baadhi ya biashara kubwa nchini Korea Kusini ikiwa ni pamoja na kampuni ya Samsung.
Park Geun-hye mwenye umri wa miaka 69 ni rais wa kwanza mwanamke aliyewahi kuchaguliwa nchini Korea Kusini. Alishinda uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2012 ambapo alimshinda rais wa sasa Moon Jae-in.
Aliungwa mkono na wahafidhina ambao walikuwa wafuasi wa baba yake aliyekuwa rais wa Korea Kusini waliyemuona kuwa ni shujaa aliyeinusuru nchi kutoka kwenye umaskini