Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 5:10 pm

NEWS: RAIS WA CHILE ANUSURIKA KUONDOLEWA MADARAKANI

Baraza la senate la Chile limemnusuru kuondolewa madarakani Rais wa nchi hiyo Sebastian Pinera mara baada ya vyama vya upinzani nchini humo kuanzisha mchakato wa kutokuwa na imani na Rais huyo, hatua ambayo Bunge la Senate limeupinga vikali na kumuweka Rais huyo huru.

Upinzani ulitaka Pinera ang’olewe madarakani kufuatia sakata lililofichuliwa kwenye nyaraka za Pandora na pia kutokana na hatua yake ya kutoshirikiana na bunge wakati mchakato huo dhidi yake ulipoanzishwa.

Waliopiga kura ili rais huyo mwenye utajiri wa Dola Bilioni 2.8 aondolewe mamlakani walikuwa 24, idadi ambayo ni chini ya kura 29 zinazohitajika ili mchakato kama huo ufaulu.

Na waliopinga kuondolewa kwake walikuwa 18. Endapo mchakato huo ungefaulu, basi huenda angekabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano gerezani.