Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 1:32 am

NEWS: RAIS WA BUNGE LA ULAYA AFARIKI DUNIA.

Rais wa Bunge la Umoja wa Ulaya David Sassoli amefariki dunia leo akiwa na Umri wa miaka 65 katika hospitali moja nchini Italia alipokuwa amelazwa tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Msemaji wa ofisi yake ametoa taarifa kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba Sassoli alilazwa hospitali kutokana na matatizo makubwa ya mfumo wa kinga ya mwili tangu Disemba 26 mwaka jana. Sassoli mwanasiasa mshosalisti kutoka Italia na mwandishi wa habari wa zamani alichaguliwa kuwa kiongozi wa bunge la Umoja wa Ulaya mnamo mwaka 2019 akiahidi kufanya mageuzi makubwa ya sera za uhamiaji ndani ya Umoja wa Ulaya.


Katika wiki za hivi karibuni Sassoli hakuonekana hadharani na hakuweza kuongoza vikao vya bunge hilo lenye viti 705 lenye makao yake mjini Strasbourg nchini Ufaransa.