- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS TRUMP AFUNGULIWA MASHTAKA NA BUNGE
Baraza la Wawakilishi nchini Marekani limepiga kura hii leo Jumatano ya kumfungulia mashtaka ya kumuondoa madarakani Rais anayemaliza muda wake Donald Trump kwa mara ya pili, hatua hii ya bunge haijawahi kutokea kwa Rais yoyote wa Marekani.
Jumla za kura zilizohesabiwa zilikuwa 232 dhidi ya 197. Warepublikan 10 waliungana na Wademokrat kupitisha uamuzi hu
Wademokrat waliowengi walimtuhumu Rais Trump kwa kuchochea mapinduzi na kuhamasisha kile kilichogeuka kuwa ni shambulizi ovu katika Bunge la Marekani.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi amemuita Trump ni tishio kwa uhuru, kujitawala na utawala wa sheria.β
Wingi mdogo wa Wademokrat katika Baraza la Wawakishi ulipata kura za kutosha kumfungulia mashtaka Trump wiki moja kabla ya muhula wake wa miaka minne kumalizika mchana wa Januari 20 na Mdemokrat Joe Biden ataapishwa kuwa kiongozi mpya wa nchi hii.