- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS SAMIA NA RUTTO WAONDOA VIKWAZO 54 VISIVYO VYA BIASHARA
Rais wa Tanzania na mwenzake wa Kenya William Ruto wamezungumza na waandishi wa habari mapema leo katika Ikulu ya Dar es Salaam, ambapo viongozi hao wawili wameahidi kuongeza ushirikiano wa kibiashara na kidiplomasia kati ya nchi mbili hizo. Rais Samia amesema, kulikuwa na vikwazo vya kibiashara 68 kati ya Tanzania na Kenya, na baada ya kufanyiwa kazi na wataalamu, vikwazo 54 ambavyo sio vya kikodi tayari vimeondolewa.
“Wataalamu wetu watavifanyia kazi vikwazo 14 vilivyobaki,” ameongeza rais Samia.
Kwa upande wake rais Ruto amesema, wakati vikwazo hivyo vikifanyiwa kazi, watu wengi walidhani vitainufaisha zaidi Kenya, lakini hii leo, Tanzania imenufaika zaidi kuliko Kenya.
Mradi wa kusafirisha gesi asilimia kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa, ingawa ushasianiwa na mtangulizi wake, lakini utakuwa ndio mradi wa kwanza kuwa chini ya usimamizi wa rais Ruto.
Rais Ruto ambae ameandamama na mke wake Rachel Ruto, pamoja na viongozi wengine, amezungumzia umuhimu wa ushirikiana wa kibiashara kati ya Kenya na Tanzania.
Ziara hiyo imejumuisha mazungumzo kati ya marais hao kuhusu masuala mbalimbali ya kimkakati kati ya nchi hizo.
Mbali na hayo, viongozi hao pia wamekubaliana kushirikiana kwa karibu na kuangalia makosa yanayovuka mpaka, madawa ya kulevya, usafirishaji haramu wa watu pamoja na ujangili.
“Nimekuja kukuhakikishia na kuwahakikishia watanzania kwamba, msingi wa ushirikiano uliojengwa kati yako na mtangulizi watu, nitauendeleza,” amesema Ruto.
Rais Samia amesema ziara ya Ruto inatoa fursa ya kutathimini fursa ya ushirikiano katika ngazi zote
“Tanzania na Kenya tusigawane umasikini na udhalili lakini tugawane utajiri tutakaofanya kupitia biashara,” amesema Rais Samia.
Kwa upande wake Rais wa Kenya, Willam Ruto amesema Serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania akibainisha kwamba, kuondoshwa kwa changamoto hizo kumeinufaisha zaidi Tanzania ikilinganishwa na Kenya.
Amesema biashara baina ya Tanzania na Kenya imezidi kuimarika ambapo usafirishaji wa bidha kwa mwaka mmoja imepanda kutoka Sh27 bilioni kutoka Tanzania kufikia Sh50 bilioni kwenda Kenya.
Kwa upande wa Kenya amesema usafirishaji wa bidhaa kutoka Kenya kuja Tanzania imepanda kutoka Sh31 bilioni kufikia Sh45 bilioni.
“Leo tunanunua vitu vingi kutoka Tanzania kuliko wanavyonunua kutoka Kenya na hii ni kutokana na ushirikiano baina ya nchi zetu.”ameeleza