Home | Terms & Conditions | Help

September 20, 2024, 9:36 pm

NEWS: RAIS SAMIA AWAKOSHA TUCTA.

DODOMA: Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi nchini TUCTA limempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua mbali mbali anazochukua katika kuboresha maslahi ya watumishi wa umma ikiwa kupandisha madaraja na kukubali ongezeka la mishahara kwa asilimia 23. 3.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma Mei 18, 2022 na Rais wa Shirikisho hilo Tumaini Nyamhokya wakati akiongeaa Waandishi wa habari ambapo amesema hatua zinazofanywa na serikali kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi zitaongeza ari ya wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na weledi.

Rais wa TUCTA ameitaka Serikali kuchua hatua kwa watumishi waliondolewa kazini wakiwemo wa darasa la saba kupewa stahiki zao.

Ameendelea kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuchua hatua kwa kutaka suala la upandaji mishahara kwa sekta binafsi lishughulikiwe.