- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS SAMIA AONGEZA KIWANGO CHA POSHA YA KUJIKIMU
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani leo ametangaza kutoa kibali cha kurekebisha posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa Watumishi wa Umma na kiwango cha malipo ya kazi maalum (Extra Duty) kwa Watumishi wa Umma nchini ambapo utekelezaji wa kibali hicho utaanza rasmi July 01,2022.
Nafuu hiyo imesemwa hii leo Mei 27, 202 na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimentu ya Utumishibwa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro Jijini Dodoma.
Dkt. Ndumbaro amesema kutokana na kibali hicho cha Rais, posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa Watumishi wa Umma kwa kiwango cha juu imepanda kutoka Tsh. 120,000 hadi Tsh. 250,000 na kiwango cha chini kutoka Tsh. 80,000 hadi Tsh. 100,000.
"Kiwango cha malipo ya kazi maalum (Extra Duty) kwa Watumishi kimeongezwa kwa ngazi zote ambapo kwa ngazi ya chini kimepanda kutoka Tsh. 15,000 hadi Tsh.30,000, ngazi ya kazi kimepanda kutoka Tsh. 20,000 hadi Tsh.40,000 na ngazi ya juu kimeongezeka kutoka Tsh. 30,000 hadi Tsh. 60,000"