- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS SAMIA AMTAKA POLEPOLE KURUDI SHULE
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemtaka aliyekuwa Mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole kurudi darasani katika chuo cha Diplomasia nchini, kwa lengo la kunolewa kwanza, kabla ya kwenda kwenye majukumu yake mapya ya ubalozi wa Tanzania nchini Malawi.
“Mheshimiwa Balozi (Polepole) najua baada ya hapa watakuweka darasani kwanza pale Chuo cha Diplomasia utakapotoka pale kabla hujaenda Malawi nitakutana na wewe, kwa hiyo tutazungumza kwa kirefu” amesema Rais Samia kwa kifupi akimuelekeza Polepole ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa mbunge wa kuteuliwa.
Agizo hilo la Rais Samia amelitoa hii leo Jumanne Machi 15, 2022 kwenye hafla ya kuwaapisha yeye Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi na Waziri Kindamba kuwa mkuu wa mkoa wa Njombe, Hafla ya kuapishwa imefanyika Ikulu, jijini Dodoma.
Awali Polepole alikuwa mbunge wa kuteuliwa ambaye aliteuliwa Novemba 29, 2020 na aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli.
Aidha kwa upande wa Waziri Kindamba ameapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, awali alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
Uchambuzi Juu ya Uteuzi wa Polepole
Uteuzi wa Polepole umeibua hisia mseto juu ya yeye kutolewa kwenye nafasi ya Ubunge wa kuteuliwa na kuwa balozi wa Tanzania nchini Malawi.
Maoni ya wananchi wengi wanaona kuwa ametolewa kwenye ubunge na kupelekwa ubalozini kama njia ya kunyamanzishwa juu ya tabia yake ya kusema sema viongozi wa Serekali hasa kupitia darasa lake la shule ya Uongozi alilokuwa akirusha kupitia mitandao ya kijamii kabla ya kufungiwa na Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA Desemba 17, 2021.
Kanuni ya teuzi za kibalozi maana yake unakwenda kuinadi au kuiuza nchi yako kimataifa juu mambo mazuri yanayopatikana nchini hata kama kutakuwa na mapungufu kwa Serekali iliyopo Madarakani, kwahiyo nafasi hiyo itamlazimisha awe ni mtu wa kuisifia Serekali muda wote ili tuwe na uhusiano mzuri na Nchi za njee pia na wawekezaji wa Malawi nchini Tanzania.
Kwa maana hiyo Polepole atalazimika kuwasema vizuri viongozi walewale aliokuwa akiwashambulia akiwaona baadhi yao kuwa ni wapigaji au alilokuwa akipenda kulitumia neno 'WAHUNI'.
Polepole amekuwa akijisifia na kujinasibu kuwa na maarifa ya Uongozi na utawala, ndio maaana akaona afungue darasa huru la kufundisha shule ya uongozi, lakini Kitendo cha leo cha Rais Samia kumwambia analazimika kwenda katika Chuo cha Diplomasia kusoma kwanza kabla ya kwenda kwenye majukumub yake mapya, maana yake ni kwamba hana maarifa ya kutosha ya uongozi na Diplomasia na alichokuwa anakifundisha kwa kipindi chote kile hakuwa na maarifa nacho.
Kufungiwa kipindi cha Shule ya Uongozi
Desemba 17, 2021 Kamati ya Maudhui ya TCRA ilisema kipindi cha Shule ya Uongozi cha aliyekuwa Mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji. Kamati imeongeza kuwa maudhui ya kipindi ni ya upotoshaji na yanayoweza kusababisha taharuki kwa wananchi.
Sasa TCRA wanasema kuwa kipindi cha Polepole cha Shule ya Uongozi maudhui yake yalikuwa ni ya upotoshwaji maana yake ni kwamba muda wote aliokuwa anafundisha alikuwa akidanganya na sio sahihi ndio maana leo mama anamlazimisha kurudi shule.
Polepole amekuwa akihusishwa pakubwa kuwepo kwenye kundi ambalo linalengo la Kukwamisha majukumu ya Mh. Rais Samia tangu ashike madaraka licha ya kukanusha mara kadhaa tuhuma hizo kupitia vyombo mbalimbali.
Sasa swali ni je Polepole ataendelea na Harakati za siasa za ukosoaji kupitia shule ya Uongozi huku akiwa Balozi au atalazimika kukaa kimya kwa muda wote mpaka astaafu kazi
Imeandikwa na Deyssa H. Issa.
Na Kuhaririwa na Merry Mgawe
Muakilishi Publisher Machi 15,2022