Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 2:10 am

NEWS: RAIS SAMIA AMSIMAMISHA KAZI DC SABAYA,KWA TUHUMA ZINAZOMKABILI

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Sabaya amesimamishwa kazi kuanzia hii leo May 13, 2021

Sebaya anatuhumiwa kufanya uvamizi kwenye makazi ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowetz kwa kutumia utambulisho wa gari la Umoja wa Mataifa(UN).

Tuhuma nyingine ni pamoja na kumdharau na kutofuata maelekezo ya Bosi wake wa kazi Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Bi Anna Mghwira.

Aidha Sabaya amewahi kutuhumiwa kumkata viongo vya mwili mmoja wa madiwani wa chama kikuu cha Upinzani Chadema katika Wilaya yake ya Hai.

Hivi karibuni Sabaya alitumia takribani Saa nzima katika kituo cha Habari cha Clouds TV kwenye kipindi cha 360 kujisafisha na Tuhuma zoote zinazomkabi.