Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 5:06 pm

NEWS: RAIS SAMIA AITISHA KIKAO CHA DHARURA USIKU WA MANANE KUPANDA KWA MAFUTA

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan usiku wkuamkia leo May 8, 2022 ameitisha kikao cha dharura katika Ikulu ya Dar es Salaam kwa lengo lakujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na Makatibu Wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza Viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la upandaji wa bei ya mafuta nchini.

Nchini Tanzania hali ya kupanda kwa bei ya mafuta kwa lita moja ya petroli kuuzwa TZS 3120 na Dizeli 3160 imekuwa ni tatizo kubwa hasa kwa wananchi wa kawaida, hali ambayo imepelekea mfumuko wa bei kuwa juu na vitu vingi kupanda bei vikiwemo vyakula kama mafuta ya kupikia na mazao ya nafaka.
mjnini Dodoma May 5 mwaka huu Wabunge wa Tanzania wameishauri Serikali kuweka ruzuku na kuondoa tozo katika mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa nchini ili kukabiliana na kupanda kwa bei za mafuta nchini.

Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma siku hiyo aliitaka Serikali kuingia gharama kuagiza yenyewe mafuta, angalau ikakubali kuingia hasara kidogo.

“Hii hali si nzuri na bado mwezi ujao yatapanda tena kwa karibu Sh3, 800, hili suala halikubaliki lazima tuone namna ya kuondoa kodi tulizoziweka katika mafuta angalau kwa miezi mitatu ili mafuta yaweze kushuka,”amesema.

Simon Songe (Busega-CCM) alisema kuwa sasa hivi gharama za kusafirisha saruji kutoka Tanga kwenda Mwanza ni Sh130,000 hadi Sh160,000 jambo ambalo litaongeza bei ya mfuko wa saruji kwa Sh1,500.