- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS SAMIA AAGIZA ALAMA YA MWENGE KUONDOLEWA DARAJA LA TANZANITE
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemwagiza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi nchini Profesa Makame Mbarawa kubadilisha alama ya mwenge iliyowekwa kwenye daraja jipya la Tanzanite lililopo kwenye bahari ya Hindi na kuweka alama ya madini hayo ili liendane na jina la daraja hilo.
Maagizo hayo ya Rais Samia ameyatoa hii leo Machi 24, 2022 jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa daraja hilo lilogharimu zaidi ya Sh 243 bilioni.
Rais Samia amefafanua kuwa ushauri huo aliupata kutoka kwa wananchi wake kwamba wangependa daraja hilo walipoweka alama ya mwenge, basi kuwekwe alama ya Tanzanite ili kuendana na uhalisia wa jina la mradi huo.
“Niseme kidogo Waziri ushauri nilioupata kutoka kwa wananchi daraja hili tunaliita la Tanzanite lakini alama tuliyoiweka ni alama ya mwenge. Pamoja na kutambua mwenge ni tunu yetu adhimu wananchi wangependa sana kuona alama ya tanzanite pale ilipo alama ya mwenge ili liendane na jina la daraja hili,” amesema Rais Samia.
Hata hivyo, Rais ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kushiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwaka huu.
“Nitoe wito kama ilivyo kawaida yangu kujitokeza kwa wingi wakati wa kuhesabiwa Agosti mwaka huu, twendeni tukahesabiwe,” amesema.