Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 4:03 pm

NEWS: RAIS MWINYI AVUNJA BODI YA WAKURUGENZI SHIRIKA LA MELI

Dar es salaam. Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi amvunja bodi ya wakurugenzi wa shirika la meli na uwakala visiwani humo.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Novemba 15, 2020 na katibu kiongozi, Dk Abdulhamid Mzee inaeleza kuwa kuvunjwa kwa bodi hiyo kunatokana na Serikali kutoridhishwa na uendeshaji na utendaji wa shirika hilo.

Jana kiongozi huyo alitengua uteuzi wa Saleh ikiwa umepita mwezi mmoja tangu alipomteua ikielezwa kuwa sasa atapangiwa kazi nyingine.
Dk Mwinyi alimwapisha Ahmed Novemba 7, 2020 katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Unguja.

“Chini ya kifungu cha Na.53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12(3) cha Sheria ya Utumishi wa umma Namba 2 ya mwaka 2011, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ametengua uteuzi wa katibu wa Rais, Suleiman Ahmed Saleh,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo ikibainisha kuwa atapangia kwazi nyingine.
Taarifa hiyo haikueleza sababu ya Rais Mwinyi kutengua uteuzi huo.