- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MWINYI AMTANGAZA OTHMAN MASOUD MRITHI WA SEIF
Dar es Salaam. Hatimaye Mrithi wa Nguli wa siasa visiwani Zanzibar Maalim Seif amepatikana hii ni baada ya leo March 1, 2021 Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi kumtangaza kada wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman kuwa Makamu wa kwanza wa Rais.
Hatua ya kutangazwa kwa Bw Othman Nguli wa Sheria visiwani Zanzibar imekuja baada ya chama cha ACT Wazalendo kukamilisha mchakato wa vikao vya kupendekeza jina la atakayerithi nafasi hiyo katika kikao kilichoketi siku ya Ijumaa Februari 26, 2021.
Taarifa iliyotolewa hii leo kwa vyombo vya habari na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Mhandisi Zena Said imesema Rais Mwinyi amezingatia kifungu cha 9(3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Kifungu hicho kinasema, ‘Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utakuwa wa Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na kutimiza lengo la kufikia demokrasia.’
Taarifa hiyo pia imesema Rais wa Zanzibar, Dk Mwinyi pia amepewa uwezo chini ya kifungu Namba 39(3) cha Katiba ya Zanzibar.
“Baada ya kushauriana na Chama cha ACT-Wazalendo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk Hussein Mwinyi amemteua Mheshimiwa Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar,” imesema taarifa hiyo.
Imesema uteuzi huo unaanza leo Machi Mosi na sherehe za kumwapisha Masoud zitafanyika kesho Machi 2 katika ukumbi wa Ikulu ya Zanzibar.