- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MUSEVENI AREJESHA SHUGHULI ZA KIUCHUMI KWA MASHARTI
RAIS wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kurejea kwa shughuli za kawaida nchini humo japo kwa masharti dhaaa huku idadi ya maambukizi ya corona nchini humo ikizidi kupanda.
Kwenye hotuba yake ya kukaribisha Mwaka Mpya, iliyopeperushwa moja kwa moja kupitia runinga za nchi hiyo, Rais Museveni alisema magari ya uchukuzi wa umma sasa yameruhusiwa kubeba idadi kamili ya abiria.
Hata hivyo, aliagiza kuwa abiria wote sharti wavae barakoa na kufuata masharti mengine ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa shule zote zitafunguliwa kuanzia Januari 10, 2022 na wanafunzi wenye umri wa miaka 18 na zaidi sharti wapewe chanjo.
Shule Uganda zimefungwa kwa karibu miaka miwili kufuatia mlipuko wa janga hilo Machi 2020.
Rais Museveni aliongeza kuwa maeneo ya burudani na michezo yarejelee shughuli za kawaida lakini sharti watu wazingatie masharti ya kuzuia msambao wa corona.
Maeneo hayo ya burudani pia yataruhusiwa kufanya kazi hadi saa za usiku.
Hata hivyo, kafyu itaendelea kuzingatiwa katika sekta ya bodaboda. Wahudumu wa pikipiki hizi za uchukuzi hawataruhusiwa kuhudumu nyakati za usiku.
Rais Museveni, hata hivyo alisema sekta nyingine za uchumi huenda zikafungwa tena ikiwa idadi ya maambukizi itaendelea kupanda